Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

62 mikoni mwa Polisi kwa uhalifu, nyara za Serikali

Image 94 1140x640.png 62 mikoni mwa Polisi kwa uhalifu, nyara za Serikali

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: dar24.com

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, linawashikilia watuhumiwa 62 kwa makosa mbalimbali wakiwepo wahalifu walio kamatwa na vifaa vya mradi wa umeme katika Bwawa la mwalimu nyerere na nyara za Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, ACP. Protas Mutayoba amesema Jeshi hilo liliendesha operesheni katika mkoa huo na kufanikiwa kukamata mtungi wa gesi uliokuwa unakwenda katika mradi huo wa mwalimu Nyerere.

Amesema, Jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata watuhumiwa wa madawa ya kulevya, pikipiki zinazotumika katika uhalifu pamoja mtuhumiwa ambaye amekutwa na nyara za Serikali.

Aidha, Kamanda Mutayoba ameeleza kuwa Jeshi hilo liliendesha operesheni ya usalama Barabarani ambapo walikamata jumla ya makosa mbalimbali 8,035huku likitoa rai kwa wananchi kutoa taarifa za uhalifu na walifu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Chanzo: dar24.com