Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

56 Walimwa faini kwa kuzamia Afrika ya Kusini

Nyundoo 56 Walimwa faini kwa kuzamia Afrika ya Kusini

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewatoza Watanzania 56 faini ya Sh50, 000 kila mmoja au kwenda jela miezi mitatu, baada ya kupatikana na hatia ya kuondoka nchini kwenda Afrika Kusini bila kufuata taratibu za Uhamiaji.

Washtakiwa hao ni Abdallah Milazi (45), Issa Kitingi (31), Shabani Shabani (27), Victor Peter (35), Seleman Limbanga (38), Yeremia Kitoka (34) na wenzao 50.

Hukumu hiyo imetolewa leo Aprili 17, 2024 na Hakimu Mkazi Mkuu Gwantwa Mwankuga, baada ya washtakiwa kukiri kosa na mahakakama kuwatia hatiani kwa kosa hilo.

Washtakiwa hao ambao walionekana wamebeba mabegi mahakamani hapo, walikiri shtaka lililosomwa na Wakili wa Serikali kutoka Idara ya Uhamiaji, Raphael Mpuya akishirikiana na Ezekiel Kibona.

Hakimu Mwankuga alisema washtakiwa wametiwa hatiani kama walivyoshtakiwa na wamekiri wenyewe shtaka lao, hivyo anawahukumu kila mmohja kulipa faini Sh50,000 na wakishindwa, watatumikia kifungo cha miezi mitatu jela kila mmoja. Awali upande wa mashtaka liomba mahakama hii itoe adhabu kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa vijana wengine. Washtakiwa hao wamefanikiwa kulipa faini na kukwepa adhabu ya kifungo cha miezi mitatu jela.

Washtakiwa walitenda kutenda kosa hilo, Aprili 11, 2024 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ( JNIA).

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, washtakiwa waliondoka isivyo halali katika ardhi ya Tanzania bila kibali kwenda nchini Afrika Kusini ambako walikamatwa na kurejeshwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live