Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

49 wakutwa na hatia kuzamia Sauzi, wapigwa faini

Hukumu Pc Data 49 wakutwa na hatia kuzamia Sauzi, wapigwa faini

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu Watanzania 49 kulipa faini ya Sh50,000 kila mmoja au kwenda jela mwaka mmoja, baada ya kupatikana na hatia ya kuondoka ndani ya Tanzania na kwenda Afrika Kusini bila kufuata taratibu za Uhamiaji.

Waliohukumiwa adhabu hiyo katika kesi ya jinai namba 30/2023 ni Mohamed Salaam, Karimu Mohamed, Mohamed Misengo, Anderson Maliki, Jackson Ramadhani, Said Kimbaka, Abdul Abas, Abdul Selemani na wenzao 40.

Hata hivyo washitakiwa hao wamefanikiwa kulipa faini na kukwepa adhabu ya kwenda kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

Hukumu hiyo imetolewa jana Alhamisi, Februari 23, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Evodia Kyaruzi baada ya washtakiwa kukiri kosa lao na mahakakama kutiwa hatiani kwa kosa hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live