Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

20 mbaroni kwa tuhuma za kuharibu basi la mwendokasi

31167 UDARTPIC TanzaniaWeb

Wed, 12 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia madereva 20 wa bodaboda kwa tuhuma za kulishambulia na kuliharibu basi la mwendokasi.

Wanadaiwa kulishambulia basi hilo baada ya mwenzao kugongwa na kufariki dunia.

Akizungumza leo Jumanne Desemba 11, 2018 Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema Desemba 8, saa nane usiku eneo la Manzese Tiptop, dereva bodaboda akiwa anapita katika barabara ya mwendokasi aliligonga basi hilo na kusababisha vifo vya watu wawili.

Amesema watu wawili waliokuwa wamepanda bodaboda hiyo walifariki dunia pamoja na aliyekuwa akiendesha.

Amesema baada ya ajali hiyo madereva hao wanaoegesha pikipiki zao kando ya barabara hiyo walianza kulishambulia basi hilo kwa mawe na kusababisha uharibifu.

Mambosasa ametoa onyo kwa madereva wote wa vyombo vya moto hususan pikipiki kuacha mara moja kutumia barabara za mabasi ya mwendokasi ili kuepusha ajali ambazo zinagharimu maisha ya watu.



Chanzo: mwananchi.co.tz