Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

193 washikiliwa kwa tuhuma uhalifu Pwani

Pinguuuuuuuu Mtu.webp 193 washikiliwa kwa tuhuma uhalifu Pwani

Fri, 5 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JESHI la Polisi Mkoa wa kipolisi Rufiji na Pwani linawashikilia watuhumiwa 193 kwa tuhuma za matukio tofauti ya uhalifu.

Akizingumza na wanahabari jana mjini Mkuranga Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga, alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika oparesheni iliyofanywa na Jeshi hilo kuanzia Mei 29.

Lyanga alisema, 156 walikamatwa wakituhumiwa kuhusika na matukio mbalimbali yakiwamo ya uvunjaji, unyang'anyi wa kutumia silaha na nguvu na wizi pamoja na utumiaji wa dawa za kulevya.

Alisema, katika oparesheni hiyo, vielelezo mbalimbali vimeanza kukamatwa ambavyo ni pikipiki sita, televisheni, deki, sabufa, kitanda cha mbao, vyoo vya kisasa viwili na simu za kiganjani mbili.

Alisema watuhumiwa wanane wameshafikishwa mahakamani na wengine watafikishwa uchunguzi ukikamilika.

Wakati huo huo, Kwa mujibu wa taarifa ya matukio kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, aliyoitoa jana mjini Kibaha, watuhumiwa 37 wametiwa mbaroni kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu.

Wankyo alisema watuhumiwa 29 walikamatwa wakiwa na mbalimbali za wizi zikiwamo televisheni tatu, pikipiki 10 ambazo zinadaiwa zimebadilishwa chesis na injini namba.

Vitu vingine vilivyopatikana kwa madai ya kuibiwa na watuhumiwa hao ni rola ya waya mali ya Tanesco, magodoro, redio, mizani ya kupimia mizigo mizito, pombe, mihadarati na mitambo ya kutengeneza pombe ya moshi.

Alisema, watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live