Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

18 wajeruhiwa ajalini

95446 Pic+ajalni 18 wajeruhiwa ajalini

Fri, 14 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kibaha.  Watu 18 wamejeruhiwa  baada ya basi walilokuwa wakisafiria la kampuni ya Saibaba kugongana uso kwa uso na lori.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa ajali hiyo imetokea jana Jumanne Februari 12, 2020  mkoani humo.

“Chanzo ni mwendo kasi wa dereva wa lori katika maeneo yasiyoruhusiwa maana alikuwa akijaribu kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake,” amesema kamanda huyo.

Amesema kati ya majeruhi hao, 16 ni wanaume akiwemo mtoto anayekadiriwa kuwa na miaka mitatu na wanawake wawili ambao majina yao hayajatambulika.

Amesema kwa sasa wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani na kwamba watano kati yao watahamishiwa Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila kwa matibabu zaidi.

Chanzo: mwananchi.co.tz