Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

17 wadakwa na Heroin, bangi na mirungi

18383 MIRUNGI+PIC TanzaniaWeb

Fri, 21 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Singida. Polisi mkoani Singida imewakamata watu 17 kwa tuhuma mbalimbali  ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin kete 741 na gramu 190, misokoto ya bangi 268 na mirungi kilo 11.

Dawa hizo za kulevya zimekamatwa katika operesheni inayofanywa katika maeneo mbalimbali mkoani hapa, lengo likiwa ni kuzuia matukio ya uhalifu, kudhibiti matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 20, 2018 Kamanda wa polisi mkoani humo, Sweetbert Njewike aliyekamatwa na Heroin ni Nurdin Mohamed (25) mkazi wa mtaa wa Majengo mjini hapa.

“Tulimhoji alikopata dawa hizo na kueleza kuwa amepewa na  Mohamed Idd (29) mkazi wa Babati mkoani Manyara. Baada ya kushirikiana na wenzetu wa Manyara tulimkamata Mohamed akiwa na kete 691 za Heroin,” amesema.

Amesema wengine waliokamatwa ni Hassan Hussein (25) mkazi wa Majengo, Hemfrey Lema (43) mkazi wa Karakana na Mwamangunwa Ibrahimu (32) mkazi wa Mromboo mkoani  Arusha kwa tuhuma ya kumiliki gramu 190 za heroin.

Kamanda Njewike amewataja Rehema Jumanne (26), Atuganile Mwangomale (30), Seleman Hassan (28) na Mwatanga Issa (21) wote wakazi wa Sekenke wilaya ya Iramba kuwa walikutwa na bangi misokoto 184.

Wengine waliokamatwa na misokoto 73 ya bangi ni Joseph Amos (23), Christpher Ally (32), Hassan Hussein (29), Eammanuel Batholomeo (34), Amosi William (19) na Mkuki Emmanuel (22) wote wakazi wa mjini Singida.

“Katika msako huo pia tumemkamata Salum Hassan (34), Selemani Hamisi (27) Ruya Salmanda (45) wote wakazi wa Arusha mjini kwa tuhuma ya kumiliki dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilogramu 11,” amesema.

Amesema baada ya upelelezi kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Chanzo: mwananchi.co.tz