Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

15 mbaroni kwa kugushi mafao NSSF

MULIRO 1.jpeg 15 mbaroni kwa kugushi mafao NSSF

Wed, 10 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imewakamata watu 30 kwa tuhuma za kughushi nyaraka zinazohusiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa lengo la kujipatia malipo ya mafao kwa njia ya udanganyifu.

Idadi hiyo ya watuhumiwa imerekodiwa katika kipindi cha miezi minne kuanzia Desemba 2023 hadi Aprili 2024, wote wakituhumiwa kufanya njama za kujipatia fedha kutoka mfuko huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumanne Aprili 9, 2024 na Kamanda wa kanda hiyo, Jumanne Muliro, watuhumiwa wamekamatwa na nyaraka bandia zinazohusu kuacha kazi, vyeti vya huduma, taarifa za uongo za ugonjwa, hati za uongo za kufukuzwa kazi na fomu za kugushi za kuomba mafao ya NSSF.

Amewatajwa waliokamatwa kuwa, Diocress Kahwa (35) mkazi wa Mbezi na mwalimu wa Shule ya Msingi Maxmilian ya Segerea; Barnabas Bonivencha na wenzake 11 wa kampuni binafsi ya ulinzi ya G4S waliowasilisha taarifa za uongo za kuacha kazi ili wapate mafao wakati bado wapo kazini.

Mwingine ni Carolina Mushi (37), mkazi wa Upanga, mtumishi wa Benki ya Stanbink akituhumiwa kughushi taarifa za hospitali za ugonjwa ili apate fao la matibabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live