Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

13 wanaotuhumiwa kutumia walemavu kushtakiwa

Dfd8feb4fdcd413d219e6c0c493d94fb 13 wanaotuhumiwa kutumia walemavu kushtakiwa

Thu, 14 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WATU 13 wanaotuhumiwa kuwatumia watu wenye ulemavu kwa kazi ya ombaomba katika maeneo mbalimbali watashtakiwa kwa makosa matano ikiwemo kutakatisha fedha haramu kinyume cha sheria na usafirisha haramu wa binadamu, kushindwa kulipa kodi na kuisababishia seikali hasara.

Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga kuhusu uamuzi wa kufungua mashtaka katika shauri hilo ulieleza kubaini watu wenye ulemavu , watoto wadogo na baadhi wakiwa ulemavu wa akili walikuwa wamehifadhiwa katika nyumba za kulala wageni zilizotambulika kwa majina ya Kolini, Madiba na Mbokomu.

Amesema nyumba hizo bubu ni mali ya Sadikiel Metta na zilikutwa na walemavu 23 kati yao wanawake nane, wanaume tisa na watoto sita ambao walikuwa wakitumikishwa katika biashara haramu ya kuomba omba mitaani.

Amesema watuhumiwa waliohusika na uhalifu huo kwa kuwasukuma walemavu kwa kutumia baiskeli maalumu ili kujipatia pesa katika biashara hiyo.

Alitaja mashtaka yanayowakabili ni kujihusisha na Uhalifu wa kupangwa na sheria ya kuzuia makosa ya uhujumu uchumi na uhalifu wa kupangwa (Sura ya 200 ya mwaka 2019), Usafirishaji haramu wa Binadamu kinyume cha sheria ya kuzuia usafirishaji Haramu wa Binadamu namba 6 ya mwaka 2008.

Pia wanatuhumiwa kuisababishia Mamlaka ya serikali hasara kinyume na sheria ya kuziia makosa ya uhujumu uchumi na uhalifu wa kupangwa, utakatishaji fedha haramu kinyume na sheria ya kuzuia Utakatishaji Fedha Haramu (sura 23 Marejeo 2019)

Anaeleza kuwa mnamo Januari mosi mwaka huu majira ya 23:00 usiku katika maeneo ya Tandale, Mtaa wa Pakacha, Polisi ilipokea taarifa ya kuwepo nyumba za kulala wageni zilizohifadhi watu wneye ulemavu kutoka mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita, Morogoro, Kagera na Tabora.

Chanzo: habarileo.co.tz