Jeshi la Polisi linawashililia watu 13 wakishukiwa kuhusika kwa mauaji ya watu sita wilayani Kilindi huku likiendelea kusaka wengine ambao wamehusika na tukio hilo.
Katika operesheni hiyo jumla ya watu waliokamatwa ni 40 na baada ya kuhojiwa 27 wameachiliwa huru huku 13 wakiendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi wamo wanaodaiwa walishiriki mauaji moja kwa moja.
Hayo yalisemwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu Dodoma na Mkuu wa Opereheni Maalumu za Jeshi la polisi Mihayo Msikhelya wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Wakati akitoa taarifa hiyo amesema pia wapo walisoshiriki kupitisha kikao cha maandalizi ya mauaji hayo ikiwemo walitoa usafiri kwa ajili ya kuwawezesha waahalifu hao kwenda kutekeleza muaji hayo.
Amesema katika operesheni hiyo walifanikiwa kukamata vielekezo mbalimbali ikiwemo silaha 11 kati ya silaha hizo 9 ni aina ya Gobore pamoja na gololi 71 ambazo zilitumika kama risasi katika Gobore hizo.
Aidha amesema silaha mbili aina ya Shotgun na risasi 10, mapanga manne kati yao moja lilitumika kutekeleza uhalifu vipande saba vya ngozi za wanyama pori na gari moja ambalo lilitumika katika kuwasafirisha wahalifu hao kwenda kutekeleza uhalifu huo.
Amesema pia gari hiyo ni aina ya Swift 1.3 yenye namba za usajili T936 CNE ndilo liliongeza nguvu kwa kuchukua kundi la wahalifu huku Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuacha kujiingiza kwenye uhalifu.
“Kwa sababu haulipi na yoyote atakayojiingiza kwenye uhalifu atashughulikiwa na kokote atakapokimbia atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria,"
Ameongeza hatua hiyo inatokana na kauli ya IGP Simon Siro aliyoitoa baada ya tukio hilo ambapo ameagiza waanze msako kwa ajili ya kuwatafuta wahalifu wa tukio hilo lilishirikisha jamii mbili za wafugaji na wakulima mzozo mkubwa ni kugombea mipaka.
Aidha baada ya maelekezo hayo kutoka kilifanyika kikao cha maridhiano kati ya wazee wa jamii ya kifugaji na wazee wa jamii ya wakulim,a na maazimio yalifikiwa kuhakikisha kabisa watoto wa shule warudi waendelee na masomo.
Amesema kwa sababu walikuwa wamekwisha kukimbia wakiamini vurugu vinaendelea lakini bado taasisi mbalimbali za serikali zinazohusika kusimamia mgogoro huo wa mpaka zinaendelea kufanyia kazi na utatuzi utapatikana wakat wowote.
Aidha Kamanda Msikelya ametoa mwito kwa wananchi kutokujiingiza kwenye uhalifu kwani haulipi na youote atayejiingiza kwenye uhalifu kokote atakapokimbili atapatikana .
Hata hivyo wanawaomba wananchi kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama wanashirikiana na kuhakikisha wanawafichukua wahusika wa tukio hilo.