Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

12 wadakwa kwa tuhuma za dawa za kulevya Tanzania

Mon, 2 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Polisi  Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya  nchini Tanzania limewakamata watu 12 wakiwa na dawa za kulevya.

Dawa hizo ni heroin zenye uzito wa kilo 4.14, kilo 31.72 za Mirungi na gramu 55.26 za bangi.

Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya cha Polisi Tanzania, Alhaj Kabaleke Salim akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Septemba 2, 2019 amesema kati ya watuhumiwa hao wanne ni raia wa Kenya, mmoja Mnigeria na tisa ni Watanzania.

Amesema watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

Chanzo: mwananchi.co.tz