Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

11 mbaroni njama za fujo Arusha

D5f8de2a9f6603bd1a9f14cba61bf353 11 mbaroni njama za fujo Arusha

Tue, 3 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limekamata watu 11 kwa makosa ya kula njama ya kufanya fujo wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Salum Hamduni alisema jana kuwa watu hao walikamatwa maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha na tayari jalada lao limefikishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Tulikamata watu 11 wakifanya fujo maeneo mbalimbali katika Jiji la Arusha na jalada lipo kwa mwanasheria wa serikali, muda wowote watafikishwa mahakamani,”alisema Kamanda Hamduni.

Alisema hakuna vurugu kwenye mkoa huo na kwamba wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku. Hamduni alisema jana hakukuwa na maandamano ya wapinzani mkoani humo na alihimiza wananchi waendelee na shughuli zao.

Wakati huohuo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limesema hali mkoani humo ni shwari na hakuna mwananchi aliyeandamana jana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Mark Njera alisema jana kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kupuuza kauli za viongozi wa vyama vya siasa na waendelee na shughuli za maendeleo.

“Maandamano hayo tulipiga marufuku kwa sababu uchaguzi umekwishafanyika, matokeo yametangazwa na viongozi halali waliochaguliwa na wananchi wametangazwa na wajibu wa wananchi kwa sasa ni kufanya shughuli za maendeleo,” alisema Kamanda Njera wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Aliwataka wananchi watii sheria na waendelee kuchapa kazi, kwa kuwa uchaguzi umekwisha. Kwa mujibu wa Kamanda Njera, uchaguzi katika mkoa huo ulifanyika vizuri na hakukuwa na tukio lolote la kuhatarisha amani.

“Zilikuwepo dosari ndogo ambazo zilizungumzwa kupitia meza ya mazungumzo na muafaka ulipatikana na hivyo kumaliza zoezi la kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa washindi,” alisema.

Kwa mujibu wa Kamanda Njera, hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kwa kosa linalohusisha uchaguzi au kuandamana. Imeandikwa na Anne Robi (Mtwara) na Veronica Mheta (Arusha)

Chanzo: habarileo.co.tz