Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

10 kortini wakituhumiwa kuvujisha mitihani darasa la saba Dar

Mitihani Picnhnhhh 10 kortini wakituhumiwa kuvujisha mitihani darasa la saba Dar

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: mwanachidigital

Watu kumi wakiwemo walimu saba wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la kusambaza mitihani ya Taifa ya darasa la saba kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Mitihani hiyo ya darasa la saba ilifanyika Oktoba 5-6, 2022.

Washtatakiwa hao ni Jonson Ondieka (37), Elinanami Sarakikya (33), Joyce Nyanyakika (50), Llyoyd Mpande (32) na Ronalda Odongo (31).

Wengine ni Dorcas Muroso (50) na Alcheraus Malinzi (47) ambao ni walimu. Aidha kuna wafanyabiashara Patrick Chawana (42) na Theresia Chitanda (37).

Akisoma hati ya mashtaka, jana Jumatano Oktoba Wakili Mkuu wa Serikali, Nassoro Katuga amedai washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka moja la kuvujisha mitihani na mawili ya kugushi.

Amedai kati ya Oktoba 2 na 12, 2022, sehemu isiyojulikana jijini Dar es Salaam kupitia mitandao ya kijamii na Telegramu walisambaza mitihani na kusababisha kuvuja kwa mitihani ya Taifa ya darasa la saba.

Katika shtaka la pili kati ya Oktoba 2 na 12, 2022 maeneo hayo mshtakiwa Malinzi akiwa na nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka za uongo wa mtihani wa somo la uraia la darasa la saba aliijifanya mtihani huo ni halali umeandaliwa na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).

Katika shtaka la tatu tarehe hiyo hiyo maeneo hayo mshtakiwa Malinzi akiwa na nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka za uongo za mtihani wa somo la Maarifa ya Jamii wa darasa la saba akijifanya mtihani huo ni halali wa Taifa umeandaliwa na Necta

Katuga amedai baadhi ya washtakiwa wengine hawajapatikana hivyo upelelezi unaendelea na kuiomba Mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo amesema dhamana ipo wazi washtakiwa wanatakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini Bondi ya Sh 5 milioni isipokuwa mshtakiwa Malinzi anayetakiwa awe na wadhamini wawili.

Hata hivyo aliyekidhi vigezo hivyo ni mshtakiwa Mpande ametoka nje kwa dhamana hivyo shauri hilo limeahirishwa hadi Novemba 2, 2022 kwa ajili ya kutajwa.

Chanzo: mwanachidigital