Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

watu 5000 Mpwapwa wanajihusisha na kilimo himilivu cha Mtama

Himilivu.jpeg Mradi unafadhiliwa na shirika la chakula duniani, WFP na serikali ya Ireland

Fri, 4 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Mradi wa Kilimo Himilivu cha Mtama katika Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kutoka Shirika la Farm Afrika Adelina Ayubu amesema kuwa zaidi ya wakulima 5000 katika wilaya hiyo wanajihusisha na kilimo hicho ambacho kimeonekana kuleta tija kubwa kwa wananchi kutoka kwenye vijiji 51, Kata 23.

Amesema hayo wilayani Mpwapwa wakati akielezea mradi huo wa mtama ambao wamekuwa wakiutekeleza kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP)pamoja na Ireland ambapo amefafanua mradi huo unatekelezwa sambamba na kutoa elimu katika vikundi vya wakulima ambapo inakuwa rahisi kuwafikia.

"Pia kupitia mradi huo, tumekuwa tukiwahusisha wakulima wa mtama kuzingatia masuala ya lishe kwa kulima bustani za mbogamboga nyumbani, lakini tunatoa elimu kuhusu namna ya kutunza mazingira kwa kutumia miti inayoitwa miti malisho.Kingine ambacho tunakifanya kupitia mradi huu ni tunawaunganisha wakulima na masoko,benki pamoja wadau wengine wa kilimo.

"Katika zana ya mikopo kwenye kutekeleza mradi kuna kipengele cha kuunganisha wakulima na hizi sekta mbalimbali ambazo si za Serikali, kwa hiyo tukaona ni vema tukashirikisha benki ili kuongeza kipato cha wakulima ambapo fedha watakazopata kutoka benki watazitumia kuandaa mashamba na mambo mengine yanayohusu kilimo.

"Kwa hiyo katika msimu wa kilimo uliopita benki ya NMB tuliwafuata kama mwanzo tu na walitusikiliza na wakatoa mikopo kwa vikundi vinne vinavyojihusisha na kilimo cha mtama, marejesho yalikuwa mazuri.Hivyo mwaka huu benki ya NMB imeamua kuongeza idadi ya vikundi ambavyo vitapatiwa fedha.Lakini tunaendelea kuzungumza na benki nyingine ikiwemo ya TADB,"amesema Adelina Ayubu.

Ameongeza mradi wa kilimo himilivu cha Mtama kinatekelezwa katika Wilaya Sita zilizopo mkoa wa Dodoma ambazo ni Kongwa, Bahi, Kondoa, Chemba,Mpwapwa na Chamwino."Kwa Wilaya ya Mpwapwa msimu uliopita tulizalisha tani za mtama mtama 13000 na bahati nzuri wakulima wengi wameelewa umuhimu wa kulima mtama, hivyo Farm Afrka na WFP tunaamini kadri mradi utakavyoendelea wengi watajiunga na kilimo hiki ambacho soko lake ni la uhakika."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live