Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

kilicho nyuma ya panda shuka bei ya mafuta

Bei Mpya Ya Mafuta Kenya Kutangazwa Leo   EPRA kilicho nyuma ya panda shuka bei ya mafuta

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza ongezeko la bei katika bidhaa za mafuta ya petroli kwa mwezi Machi, 2024 ambalo limechangiwa na matumizi ya EURO katika kulipia mafuta yaliyoingizwa nchini.

Pia Ewura imesema mabadiliko hayo yamechangiwa na ongezeko la bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia (FOB) kwa wastani wa asilimia 4.5 kwa mafuta ya petroli, asilimia 1.99 kwa mafuta ya dizeli na gharama za premium kwa bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga.

Bei mpya zinazoanza kutumika leo Machi 6 ni Sh 3,163 kwa lita ya Petroli, Sh 3,126 kwa lita ya Dizeli na Sh 2,840 kwa lita ya Mafuta ya Taa yaliyoingizwa kupitia bandari ya Dar es Salaam. Bei hii ni ongezeko la Sh 75 kwa lita ya petroli kutoka Sh 3,051 kwa lita mwezi Februari. Bei ya Dizeli ilikuwa Sh 3,029 na bei ya mafuta ya taa ilikuwa Sh 2,840 kwa lita.

Bei kikomo kwa mafuta yaliyoingizwa kupitia bandari ya Tanga kwa sasa itakuwa Sh 3,209 kwa lita ya Petroli, Sh 3,173 kwa lita ya Dizeli na Sh 2,886 kwa Taa. Huko Mtwara, lita ya petroli itakuwa Sh 3,155, lita ya Dizeli Sh 3,070 na lita ya mafuta ya taa ni Sh 2,913.

Tofauti na maeneo mengine, bei ya petroli huko Kyerwa (Ruberwa) mkoani Kagera ni Sh 3,401 kwa lita, dizeli Sh 3,364 na mafuta ya taa Sh 3,078 kwa lita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live