Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zungu awapa mbinu wafanyabiashara Kariakoo

Zungu Er Zungu awapa mbinu wafanyabiashara Kariakoo

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Spika wa Bunge Mussa Azan Zungu amewataka wafanyabishara wa Kariakoo kuendana na maendeleo ya teknolojia kwa kufanya biashara zao mitandaoni na wasisubiri wateja wawafuate.

Zungu amesema dunia imekua kiteknolojia hivyo siyo lazima mtu afunge safari kufuata bidhaa Kariakoo kwa kuwa teknolojia inaruhusu mteja kufikishiwa bidhaa popote alipo.

Naibu Spika ambaye pia ni mbunge wa Ilala ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, Oktoba 9, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akizindua kampuni ya Tamim Star Cargo inayosafirisha bidhaa kutoka China na kutoa ushauri wa kibiashara.

New Content Item (1)

Amesema wafanyabiashara bila kujali ukubwa wa shughuli zao wanapaswa kujiongeza kwa kuipa nafasi kubwa teknolojia kwa matumizi yao kuwa dunia ndiko iliko kwa sasa.

“Tuitumie teknolojia vyema, huna sababu ya kukaa na bidhaa zako Kariakoo unasubiri wateja waje. Jiongeze tangaza huko mitandaoni wapelekee watu bidhaa nyumbani. Msikae kulalamika wateja hakuna wakati zipo njia za kuwafikia.

“Kinachofanywa na kampuni hii ni kuzidi kurahisisha ufanyaji biashara, sio lazima wewe ufunge safari kwenda China unaweza kuwa na mtaji mdogo ukaagiza bidhaa na ukatumia teknolojia kuziuza hapa maisha yakaendelea,” amesema Zungu.

Pia amezitaka benki kutoweka masharti magumu ya mikopo kwa vijana na wanawake kwa kuwa kundi hilo lina uhitaji mkubwa wa kukuza biashara ila wakati mwingine linakwamisha na masharti magumu ya taasisi za fedha.

Zungu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha vijana hasa wa kike kuacha kuhangaika na vitu vya anasa vinavyowagharimu fedha nyingi ambazo wangeweza kuzitumia kama msingi wa biashara.

“Dada zetu lazima tuseme ukweli hakuna haja ya kuwa na simu za gharama ili muonekane wazuri. Acheni mambo ya kishamba muhimu ni kuwa na mawasiliano. Sh5 milioni unaweza kuitumia kufanya biashara. Tuache mambo ya anasa kununua simu au nywele kwa fedha nyingi ambazo ni msingi kabisa wa biashara,”amesema Zungu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Tamir Star Cargo, Tamim Ahmed amesema tofauti na ilivyo kwa kampuni nyingine za usafirishaji hiyo itajikita pia katika kutoa elimu kwa wajasiriamali wadogo.

“Nimekaa China kwa miaka 18 hivyo nina uzoefu wa kutosha katika eneo la biashara, ndiyo maana kampuni yetu haitaishia kusafirisha mizigo bali kuwapa elimu wajasiriamali wadogo ili waweze kukuza biashara zao.

“China hata ukiwa na kiasi kidogo cha fedha inaweza kuwa mtaji wa kutosha kufanya biashara ukanunua bidhaa ukaja kuziuza Tanzania, hata haya mambo ya vijana kuwa na simu za gharama yanashangaza kwa kuwa wanatembea na mitaji ya biashara,” amesema Tamim ambaye pia ni mwenyekiti wa diaspora wa Tanzania nchini China.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live