Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto asema uchumi unakua kwa wachache

Uchumi Kupanda Zitto asema uchumi unakua kwa wachache

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa uchumi wa Tanzania unakua vizuri, lakini changamoto kwenye historia ya ukuaji wake unakuwa zaidi kwenye sekta ambazo zinaajiri Watanzania wachache.

Akizungumza jana Aprili 19, kwenye mjadala ulioendeshwa kupitia Mwananchi Twitter Space, uliohoji ‘Ukuaji wa pato la Taifa unaendana na uchumi wa Wananchi?’ Zitto ametolea mfano sekta za madini, mawasiliano na utalii zinazoajiri watu wachache.

“Changamoto kwenye historia ya ukuaji wake unakuwa zaidi kwenye sekta ambazo zinaajiri Watanzania wachache, mfano sekta ya madini, mawasiliano na utalii ambazo zina watu wachache lakini, zimekuwa na umuhimu mkubwa kwenye kukuza pato la Taifa,” amesema.

Zitto amesema Kasi ya ukuaji wa pato la Taifa ni matokeo ya kuongezeka kwa uzalishajii wa shughuli za Wananchi.huku akitolea mfano idadi ya watalii ikiongezeka uzalishaji katika sekta ya hiyo utaongezeka.

Naye Mchambuzi, Robert Mwaura ameshauri umuhimu wa Serikali kuangalia namna ya kutengeneza mazingira rafiki kwa biashara ndogondogo na zile za kati zikue kule unafuu wa maisha kwa Wananchi.

“Shida Tanzania kuna watu wana hela lakini ni wachache, Serikali iangalie itengenezea mazingira rafiki kwa biashara ndogondogo na za kati zikue.

“Kwa mfano nchi nyingine katika kila Sh10 ambayo Serikali inakusanya, unakuta Sh9 inazipata kutoka kwa biashara ndogondogo na za kati,” amesema.

Chanzo: mwanachidigital