Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto aishauri TANESCO kuuza hisa DSE

Zitto (600 X 337) Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu ACT

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasiasa na Mchumi Zitto Kabwe ameitaka Serikali kuorodhesha walau asilimia 20 ya hisa za Shirika la Umeme nchini TANESCO kwenye Soko Kuu la Hisa la Dar es Salaam DSE kama njia ya kurekebisha na kuboresha mfumo wa shirika hilo kiutendaji.

Majibu ya Serikali katika wazo hilo yalikuwa ya moja kwa moja bila kupepesa macho, kupitia Waziri wa Nishati January Makamba ambaye alisema kuwa Serikali haina mpango wa kufanya kama ambavyo Zitto ameshauri.

"Hapana, hatuna mpango kabisa wa kutangaza kuuza hisa za Shirika la Umeme popote pale" amesema Makamba.

Makamba ameongeza kusema kuwa nia ya Serikali(Mmiliki mkuu wa hisa za TANESCO) ni kutaka kuiona TANESCO ikiwa imepangwa katika mifumo rafiki kiutendaji.

"Kama mmiliki mkuu wa hisa, sisi kama Serikali tumetaka tu kuiona TANESCO ikiwa imepangwa vizuri kama Taasisi, ikitoa huduma nzuri, ikiongeza idadi ya wateja, ikiwa na uchumi imara na kusaidia kuongezza pato la taifa" Amesema Makamba.

Lakini kwa mujibu wa Zitto ni kuwa kuweka hisa za TANESCO sokoni kutasaidia kuongeza mapato ya shirika hilo sambamba na kupunguza hasara ambazo nyingi hutokana na ukosefu wa ufanisi katika maeneo ya kazi.

Hata hivyo ushauri huu ni kwa mujibu wa kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Maharage Chande, aliyesema kuwa TANESCO inapoteza zaidi ya dola milioni 7 sawa na bilioni 16.13 za kitanznaia kwa mwezi kufuatia upotevu mkubwa wa nishati unaosababishwa na sababu za kiufundi na zisizo za kiufundi kwa maana ya sababu za kiutendaji.

Zitto amesisitiza suala la kuuzwa kwa hisa hizo kwa kusema kuwa utaratibu wa DSE upo kwa uwazi, hivyo itakuwa rahisi sana kwa shirika hilo kufanya tathimini pindi ripoti za wiki, mwezi zikitolewa na DSE.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live