Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ziara ya Mkenda Burundi neema kwa wakulima nchini

Mkenda Pic Waziri Mkenda atembelea kiwanda cha mbolea Burundi

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo, Prof.Adolf Mkenda yupo jijini Bunjumbura nchini Burundi kwa ajili ya ziara ya kikazi na tayari ametembelea kiwanda kikubwa cha kuzalisha mbolea cha nchini humo.

Ziara hii imekuja kufuatia ujenzi wa kikwanda kikubwa cha mbolea cha Itracom Fertiliser Limited unaofanyika eneo la Nala lilipo jijini Dodoma.

Hata hivyo inaelezwa kuwa Itracom inamilikwa na kiwanda cha FOMI alichotembeea Waziri Mkenda Oktoba 20, 2021.

Kiwanda cha Itracom kinatarajiwa kuja kuwa mkombozi kwa wakulima nchini, hasa ikizingatiwa kuwa sio tu kwamba kitatengeneza ajira 3,000 bali kitakuwa kikizalisha zaidi ya tani 600,000 za mbolea asilia kwa mwaka.

Uzalishaji huo utapanda kutoka tani 400,000 kwa 500,000 zinazozalishwa hivi sasa kwa mwaka mzima.

Ujenzi wa kiwanda hicho unagharimu dola milioni 180 sawa na milioni 414.0 za kitanzania na kitakamilika mwezi August 2022.

Hadi saa Tanzania inaagiza zaidi ya asilimia 90 ya mbolea kutoka nje, jambo ambalo limeifanya Serikali kuwekeza katika ujenzi huo.

Hivyo ziara hii ya Waziri Mkenda inatarajiwa kufanya mapinduzi kwani kwa mujibu wa Waziri huyo ni kuwa hadi sasa ameshabadilishana mawazo na wataalum wa uzalishaji wa mbolea nchini Burundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live