Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zao la utomvu laiingizia Saohill Sh700 milioni

Thu, 23 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mufindi.  Shamba la miti la Sao hill limekusanya zaidi ya Sh700 milioni katika kipindi cha miezi 10 kupitia zao la utomvu huku likikusanya zaidi ya Sh47 bilioni katika uvunaji wa miti kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

 

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, David William wakati wa ziara ya kikazi ya  wakuu wa wilaya  ya Namtumbo, Nyasa na Songea za mkoani Ruvuma na wadau wa shamba la miti Mpepo lililopo mkoani humo walipotembelea shamba la miti la Saohill.

 

Taarifa iliyotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) ambao ndiyo wasimamizi wa shamba hilo,  imeeleza kuwa mkuu huyo wa wilaya ameridhishwa namna shamba hilo linavyosimamiwa.

 

Pia Soma

Amesema kazi kubwa inayofanywa na uongozi wa shamba hilo kuhakikisha kuwa rasilimali hiyo inaendelea kuchangia katika ukuaji wa uchumi, kuwaongezea wananchi kipato na kuongeza fursa za ajira.

 

Kaimu meneja wa Saohill, Daniel Silima amesema katika kipindi cha mwaka 2008 hadi 2019, shamba hilo limeweza kukusanya zaidi ya Sh319bilioni, na  Sh6 bilioni kama mrabaha wa mauzo ya miti (CESS)  kwa halmashauri za Wilaya ya Mufindi, mji wa Mafinga na Kilombero.

 

Kiongozi wa msafara huo, Mkuu wa Wilaya ya Nyansa, Isabela Chilumba amesema waliamua kufanya ziara ya kujifunza shambani hapo kutokana na mafanikio yake katika sekta ya misitu na ufugaji nyuki.

 

Katika ziara hiyo  walipata fursa ya kuona shughuli za ufugaji nyuki na kiwanda kidogo cha kuchakata asali,  kutembelea bustani ya miti, ugemwaji wa utomvu na kutembelea viwanda vya kuchakata mazao ya misitu ili kujionea kazi mbalimbali zinazofanyika katika shamba hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz