Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zao la Mkonge kupanda thamani

713eb9a9d02142c7d517b99ab072728f Zao la Mkonge kupanda thamani

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Katika kulipa thamani zao la mkonge nchini, Kampuni ya Grosso Sisal Limited’ ya nchini Uholanzi ipo katika mchakato wa kuwekeza Sh bilioni 13.8 kwa ajili ya usindikaji wa zao hilo mkoani Tanga.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Nurdin Osman amesema wameamua kufanya hivyo kama njia ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza thamani ya zao hilo.

Amesema kampuni hiyo itazingatia utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zitakazotokana na zao hilo ikiwemo nyuzi zitakazokidhi ubora wa viwango vya soko la kimataifa. “Tafiti zinaonesha ni asilimi mbili tu ya Mkonge unaozalishwa nchini Tanzania ndio unaendelezawa huku asilimia 98 ikiachwa ikipotea hivyo tumeamua kuwekeza katika kilimo hiki” amesema Osman.

Chanzo: habarileo.co.tz