Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar yatoa msamaha wa kodi kwa wajasiriamali

Tax Tax Ushuruuuu Zanzibar yatoa msamaha wa kodi kwa wajasiriamali

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameagiza kusamehewa kwa kodi ya miezi mitatu kwa wajasirimali walioanza mauzo ya biashara zao katika eneo jipya la Kituo cha Wajasirimali Chake chake Kusini pemba ambacho kimegharimu Zaidi ya shilingi Bilioni moja

Rais Dkt Mwinyi ameeleza hayo wakati alipozindua kituo cha wajasiriamali katika wilaya ya Chakechake Pemba ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuadhimisha miaka mitatu ya uongozi wake tangu aapishwe kushika nafasi hiyo.

Aidha ameagiza baraza la manipaa kuhakikisha hawaruhusu wafanyabiashara kufanya biashara zao katika maeneo yasiyo rasmi ikiwemo pembezoni mwa barabara sambamba na kuziagiza mamlaka zinahusika kuendeela kutoa fursa kwa wajasiriamali kupata mikopo ili kujiimarisha kibiashara

Kituo hicho cha wajasirimali kimetoa fursa ya kuwepo kwa maduka pamoja na vibaraza vitakavyowawezesha wajasiriamali Zaidi ya mia na hamsini kunufaika na mradi huo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live