Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar yatangaza vitalu 12 utafutaji mafuta gesi asilia

Gesiii Zanzibar yatangaza vitalu 12 utafutaji mafuta gesi asilia

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya shughuli ya kuchakata data za mafuta na gesi, Zanzibar kwa mara ya kwanza Zanzibar imetangaza maeneo mapya ya kutafuta rasilimali hiyo kisiwani humo.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iliingia mkataba na kampuni ya kimataifa ya Schlumberger kuchakata data za mafuta na gesi ambapo utekelezaji wake ulitarajiwa kukamilika Juni mwaka huu.

Agosti 10, 2022 Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPRA) ilikabidhiwa rasmi data hizo kutoka Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu (Pura).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 31, 2023 mijini Unguja, Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Suleiman Masoud Makame amesema kazi ya kuzichakata data hizo imekamilika sasa unaanza utaratibu wa kugawa maeneo mapya ya bahari kuu ya Mashariki ya Zanzibar katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Kuna jumla ya vitalu 12

“Hatua hiyo inafungua awamu mpya ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia ambao una lengo la kukuza sekta hii kwa kufungua fursa kwa wawekezaji wa utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kuomba maeneo hayo kupitia Zabuni ya Kimataifa itakayotangazwa kabla ya kumalizika mwaka 2023,” amesema.

Amesema SMZ inazikaribisha kampuni za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kuangalia data za Zanzibar na kuanza kupendekeza maeneo yanayowavutia zaidi katika kuwekeza kabla ya kuanza kwa zabuni hiyo.

“Zabuni hii ni zabuni ya kwanza kwa Zanzibar katika masuala ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ikiwa ni moja ya shughuli katika mpango wa miaka mitano wa uendelezaji wa sekta hiyo kisiwani hapo,” amesema Waziri Masoud.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa data hizo Agost 10, 2022, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi alisema kuna kila dalili inayoonyesha Zanzibar ina rasilimali ya kutosha ya mafuta na gesi.

“Mungu atatuwezesha Zanzibar sasa ianze kuchimba mafuta na gesi, kila dalili zipo za kuwa na rasilimali ya kutosha kilichobaki ni kukamilisha kutoka hapa kwenda hatua nyingine.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 34 cha Sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na gesi asilia ya mwaka 2016, waziri anayehusika na masuala hayo, atatangaza juu ya ufunguzi wa maeneo mapya ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kabla ya kuanza kwa shughuli hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live