Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar yafanya mapinduzi ya kidigitali kukuza Uchumi

Saudia.png Zanzibar yafanya mapinduzi ya kidigitali kukuza Uchumi

Mon, 27 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imebainisha dhamira yake ya kuhakikisha wanakuza uchumi wa kisasa unaoendana na falsafa ya uchumi wa kidijitali na uchumi wa bluu kwa kuboresha huduma za TEHAMA.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Zanzibar Amoul Hamil wakati akikabidhi kituo cha Kompyuta kwa Umma (Tele-Center) kwa Skuli ya Sekondari Tumbatu kilichojengwa kwa udhamini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa shabaha ya kutoa huduma za TEHAMA kwa walimu,wanafunzi na jamii ya kisiwa kidogo cha Tumbatu.

"Sasa tunaelekea kutimiza dira za maendeleo ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Serikali ya Zanzibar,katika kuhakikisha kuna kuwepo na matumizi bora katika teknolojia ya habari ili kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kidigitali" Amesema Katibu Mkuu huyo.

Nao TCRA wamesema kuwa lengo la kutekeleza suala hili la TEHAMA kuwafikia wananchi wote ni kuwezesha mapinduzi ya uchumi wa kidigitali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live