Mwezi ujao, Zanzibar inatarajiwa kuwa mwenyeji Kongamano la Wawekezaji wa Taasisi za Afrika Mashariki na Kati, litakalozingatia uwekezaji wenye tija, Kongamano hiyo litafanyika mwezi Februari mwaka 2023.
Kongamano hilo la siku mbili lenye kauli mbiu ya "Kutafakari Marudio ya Uwekezaji katika Mfumo Mpya wa Kawaida, Uwekezaji wenye tija" iliyopangwa kuanza Februari 22, itawaleta pamoja wadau kujadili masuala mbalimbali yanayohusu kuchangia maendeleo endelevu ya kiuchumi ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa kuvutia uwekezaji mpya na kuongeza tija kwa uchumi.
“Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo kwa kuwa ni kivutio cha uwekezaji kinachozidi kuwa maarufu na kuonyesha ukuaji wa juu. pia utulivu wa kisiasa na imeweka vivutio mbalimbali vya kukuza uwekezaji,” ilisema taarifa ya MNCapital Group, kampuni ya uwekezaji yenye makao yake makuu Afrika Kusini inayoandaa hafla hiyo.
Kwa mujibu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, baadhi ya sekta zenye faida kubwa zinazotoa matarajio ya uwekezaji nchini ni pamoja na kilimo, mifugo, viwanda, miundombinu ya kiuchumi, madini, utalii, afya, elimu, TEHAMA na ukuzaji wa ufugaji wa samaki.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Michael Ndinisa alisema; "Katika ulimwengu wa baada ya janga la UVIKO-19 dunia yote kwa ujumla inapambana kufufua uchumi ili kupunguza changamoto za kijamii na kiuchumi ambazo zinaweza kuwa zimesababishwa au hazijasababishwa na janga hilo".
Alisema mkutano huo utatoa fursa kwa wawekezaji wa taasisi kufanya uwekezaji wenye tija kwa kijamii pamoja na kupata faida inayotarajiwa kwenye uwekezaji.