Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar kununua boti 2 za abiria

Boti Mbili Utalii Zanzibar kununua boti 2 za abiria

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)ipo kwenye mchakato wa kununua boti mbili za mwendo kasi zitakazofanya safari kati ya Unguja, Pemba, Tanga na Dar es Saalam, ili kukabiliana na changamoto ya usafiri majini.

Pia inaendelea kufanya matengenezo makubwa ya meli ya Mv Mapinduzi II yanayotarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Khali Salum Mohamed wakati wa uzinduzi wa boti mpya ya Kampuni ya usafiri wa baharini Azam Marine-Kilimanjaro Fast Farries ya Kilimanjaro VIII katika bandari ya Malindi ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Hussein Mwinyi

“Serikali ipo kwenye mchakato wa kununua speed boti mbili kwa ajili ya usafiri baina ya Unguja Tanga na Pemba, kwa hiyo tatizo la usafiri linalozungumzwa litakuwa limepatiwa ufumbuzi,” alisema. Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Mwinyi alisema Serikali inaimarisha sera ya uwekezaji kwa kuwavutia watu binafsi kuwekeza katika usafiri wa baharini.

Alisema katika kukabiliana na mahitaji ya kuwa na vyombo vya usafiri wa baharini vya kisasa vyenye kuzingatia usalama wa abiria na mizigo, Serikali imekuwa ikiwahamasisha wawekezaji binafsi kutumia fursa hiyo.

“Kwa hakika, mchango wa kampuni binafsi ni mkubwa sana kurahisisha huduma za usafiri wa baharini kati ya bandari za Unguja, Pemba na Dar es Salaam.

“Serikali inatambua kuwa kuimarika kwa sekta ya usafiri wa baharini, kunategemea kuimarika kwa huduma zinazotolewa katika bandari hivyo licha ya changamoto mbalimbali, Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuimarisha huduma za bandari ya Malindi inayotumika kwa usafiri huo,” alisema.

Awali, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kukuza uwekezaji na vitega Uchumi (Zipa), Shariff Ali Shariff alisema kampuni ya Bakhresa ilianza kuwekeza katika mradi huo mwaka 2016, una thamani ya Dola za Marekani milioni 120 na imetengeneza ajira 281.

Kati ya hizo ajira hizo, 222 ni Wazanzibari, huku wanaume wakiwa 182 na wanawake 40. Akitoa maelezo ya mradi huo kwa niaba ya kampuni ya Azam Marine, Abubakar Aziz, alisema kampuni imetoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 400 na husafirisha abiria milioni mbilil kwa mwaka kati ya Zanzibar na Tanzania bara.

Boti hiyo mpya imejengwa kwa miezi 18 nchini Australia na ina uwezo wa kubeba abiria 631.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live