Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar kufanya hivi kupunguza ugumu wa maisha

046ae6036c5877aa552c43497811196b.PNG Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema inatoa kiasi cha Sh bilioni tatu kila mwezi kwa ajili ya kufi dia gharama za mafuta. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi alisema hayo jana Ikulu ya Zanzibar alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Dk Mwinyi alisema kutokana na matukio kadhaa yanayotokea duniani ikiwemo vita kati ya Urusi na Ukrane hali ya uchumi wa dunia imeyumba na kusababisha kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema serikali imeamua kufidia ongezeko la bei za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa kutoa kiasi hicho cha Sh bilioni 3 kila mwezi na kupunguza ushuru wa bidhaa za vyakula ikiwemo sukari, ngano na mafuta ya kula.

Dk Mwinyi alisema hatua hizo zitachukuliwa kulingana na uwezo wa serikali na hakuna muda maalumu wa utekelezaji uliopangwa kwa sababu haijulikani tatizo hilo litachukua muda gani.

“Kwa upande wa chakula hatufidii fedha ila tumepunguza ushuru na ndiyo maana tumeweka bei elekezi za bidhaa, huwezi kuweka bei elekezi kama hujapunguza mzigo wa ushuru hivyo tumepunguza na kuweka bei elekezi, nalo tutakwenda nalo kwa muda gani itategemea na uwezo wa serikali. Hakuna muda maalumu tulioweka isipokuwa uwezo wa serikali utaamua tunaweza kuendelea kwa muda gani,” alisema.

Dk Mwinyi alitoa mwito kwa wananchi wazingatie kulipa kodi iliyobaki kwa ukamilifu na mamlaka husika ziwe makini kukusanya mapato ili serikali iweze kuhudumia wananchi na kutekeleza hatua hizo vizuri.

Dk Mwinyi alisema wako katika harakati za kukutana na waajiri katika sekta binafsi watafute njia za kuwasaidia wafanyakazi wamudu gharama za maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live