Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar kuendelea kushirikiana na Norway

Zamzibar Na Norway Zanzibar kuendelea kushirikiana na Norway

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar itaendelea kushirikiana na Serikali ya Norway katika sekta mbalimbali.

Rais Mwinyi amesema hayo leo Mei 30, 2024 alipokutana na Balozi wa Norway nchini, Tone Tinnes aliyefika Ikulu Zanzibar kujitambulisha.

Aidha, Dk.Mwinyi amemueleza Balozi Tinnes kuwa Zanzibar imeendelea kunuifaika na fursa nyingi kutoka Norway na ipo tayari kuendeleza ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati ya umeme kuwajengea uwezo watendaji wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).

Pia, Sekta ya mazingira, utalii, afya, elimu, Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), Mafuta na Gesi.

Naye, Balozi Tinnes amesema Norway itaendelea kudumisha uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia uliopo na kuendeleza ushirikiano kwenye sekta mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live