Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar imetangaza fursa ya uwekezaji kwenye visiwa hivi

Zanzibar Island Vijue Visiwa vidogo Zanzibar vinavyohitaji wawekezaji.

Thu, 26 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania Bara na visiwani Zanzibar imewataka wawekazaji kuwekeza, kuendesha na kuviendeleza visiwa 9 vilivyopo Unguja na Pemba.

Tangazo hilo linatolewa Sambamba na jukumu la Zanzibar katika kukuza uchumi. Zanzibar pia inakusudia kukuza zaidi maendeleo ya visiwa vyake vidogo, vijikite katika shughuli za uchumi kwa kiwango cha juu.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya Zanzibar inasema;"Uamuzi huo umefikiwa ili kuvutia wawekezaji kwa kiwango kikubwa. Visiwa vidogo vinavyoizunguka Zanzibar ni hazina nzui ambayo mwekezaji anaweza kupata faida kubwa"

Serikali ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya kukuza uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imewaalika wawekezaji kuweka wazi mikakati ya kuviendeleza visiwa, namna watakavyoviendesha, na kusimamia visiwa hivyo vidogo.

Kwa mujibu wa ZIPA wawekezaji watakaohitaji kuwekeza wanatakiwa kutoa taarifa za uzoefu wao katika kuwekeza, kukuza na kusimamia miradi ya uwekezaji, uwezo wao wakutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na ujuzi na uzoefu wao katika masuala ya utamaduni na maendeleo ya jamii ya watu waishio visiwani hadi kufikia septemba 16.

Baadhi ya Visiwa Vidogo vilivyopo sokoni tayari kwa kuwekeza huko Unguja ni Changuu, Bawe, Pamunda A na B, Kwale na Chumbe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live