Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar: Tuna uhaba wa pombe

Bia Pombe Alcohol Scaled Zanzibar: Tuna uhaba wa pombe

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utalii na mambo ya kale Zanzibar Simai Mohammed Said amesema kuna athari zimeanza kujitokeza na kuzua sintofahamu ya kurudisha nyuma biashara ya utali Zanzibar kufuatia uhaba wa pombe katika Hoteli na Migahawa mbalimbali ya Watalii Visiwani humo.

Waziri Simai amesema yapo malalamiko mengi yaliyotolewa na Waendeshaji wa Hoteli hizo wakidai kwamba baada ya Bodi ya Vileo ya Zanzibar kufanya maamuzi ya kubadilisha Mawakala wa kusambaza vileo hivyo uhaba huo umeanza kuonekana.

Waziri wa Utali ameyasema hayo baada ya kikao cha dharura na Wadau wa Sekta ya Utalii kufuatia malalamiko waliyoyatoa Wadau wa Migahawa na hoteli za Kitalii kwa Uhaba wa Vinywaji kwa Watalii.

“Masikitiko yamekua makubwa na imenibidi niitishe kikao kwa sababu nimeanza kunyooshewa mkono na Wadau, mimi kama Baba wa Mahoteli na Migahawa lazima nionane nao kwani Sekta ya utalii si vyema ikachezewachezewa.

“Tumeona maamuzi ya Bodi ya Vileo Zanzibar imewaondosha wale waliokua wanahusika kama ZMMI, Scoch na One Stop, nimeanza kuona athari hoteli nyingi wameanza kukosa huduma ya Vinywaji baada ya Bodi ya Vileo kufanya maamuzi hayo, niwaombe Wawekezaji waendelee kuwa Wavumilivu wakati huu ikitazamwa namna ya kutatua jambo hili,” amesema Waziri Simai.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live