Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar, Oman kuibua fursa uwekezaji

OTHMAN OMAN Zanzibar, Oman kuibua fursa uwekezaji

Fri, 3 Sep 2021 Chanzo: ippmedia.com

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema Zanzibar na Oman zinaweza kutumia historia na uhusiano wa damu uliopo wa muda kuibua fursa mpya zaidi za uwekezaji ili kusaidia kukuza uchumi na maendeleo ya kijamii.

Othman aliyasema hayo ofisini kwake, alipozungumza na Balozi mdogo wa Oman, Said Salim Al Sinawi.

Alisema yapo maeneo mengi ambayo yanaweza kujadiliwa zaidi na baadaye kujengewa ushirikiano unaoweza kusaidia manufaa kwa Zanzibar na Oman.

Pia alimueleza Balozi Al Sinawi kwamba suala la Mahakama ya Kadhi, fursa za masomo na kubadilishana uzoefu ni miongoni mwa maeneo muhimu, ambayo serikali hizo mbili zinaweza kujadiliana na kukubaliana kuongezwa ushirikiano kwa kuwa yana mchango mkubwa katika historia Oman na Zanzibar.

Alisema Oman ina uzoefu mkubwa katika kusimamia mahakama za kadhi na kwa vile ni waanzilishi wa mahakama hiyo Zanzibar ni muhimu kuongeza ushirikiano katika kusaidia mbinu za uendeshaji na usimamizi wa hakama hizo Zanzibar.

Alisema Oman imekuwa na mchango mkubwa katika uanzishwaji wa mahakama hizo sio tu kwa Zanzibar, lakini na nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwamo Kenya na Uganda.

Othman alimweleza Balozi huyo kwamba hivi sasa Zanzibar inatekeleza sera yake ya Uchumi wa Bluu, na imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo yanaweza kutumika kama fursa ya kuendeleza uwekezaji na kusaidia nchi kukuza uchumi.

Naye Balozi wa Oman, Said Salim Al Sinawi, alisema Oman ipo tayari kuendeleza ushirikiano wa historia uliopo katika sekta mbalimbali na kwamba anaichukulia Zanzibar kuwa ni nyumbani kwao kutokana na udugu wa damu uliopo kwa muda mrefu.

Aidha, alisema serikali ya Oman ina nia thabiti ya kusaidia Zanzibar na Tanzania kwa jumla katika maeneo mbalimbali, licha ya UVIKO-19 kuwa kikwazo katika utekelezaji wa mambo mbalimbali hivi sasa.

Alisema nchi yake na Zanzibar tayari inamakubaliano ya ushirikiano wa kuendeleza sekta ya biashara ya utalii ambayo inasaidia sana kukuza uchumi na maendeleo.

Chanzo: ippmedia.com