Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) zimeingia makubaliano ya kushirikiana katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwa kipindi cha miaka mitatu.
Makubaliano hayo yamesainiwa leo, Alhamisi Mei 11,2023, jijini Dodoma na Katibu Mtendaji wa NEEC, Being'i Issa na Mkurugenzi Mtendaji wa ZEEA, Juma Amour Mohammed.
Katibu Mtendaji wa NEEC,Being'i amesema watashirikiana kwenye utafiti,sera za uwezeshaji pamoja na kufanya tathmini kwenye mambo ambayo watashirikiana.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa ZEEA, Mohammed amesema wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar ni taasisi mpya ambayo ina umri wa mwaka mmoja ambao wamefanikiwa kutekeleza majukumu yake kiufasaha kwa kutoa mafunzo mikopo kwa wananchi zaidi ya 18,493.