Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zantel sasa yazindua kampeni yake upya

Pics Pg 17 Mei 21 Zantel sasa yazindua kampeni yake upya

Fri, 21 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Kampeni hiyo inayohusisha shughuli mbalimbali za uelimishaji, ilisimama kwa muda kupisha mambo kadhaa ikiwamo mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.   Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika viwanja vya Gombani Kongwe visiwani Pemba, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Zantel, Aneth Muga, alisema lengo kubwa ni kuhakikisha wateja wananufaika zaidi na matumizi ya intaneti mbali na matumizi ya mitandao ya kijamii.   “Leo tunafuraha kuwajulisha wateja wetu kuwa tumerudi tena na kampeni yetu hii mahsusi ili kuendelea kutoa elimu kwa wateja wetu juu ya manufaa mbalimbali yatokanayo na mtandao ulioboreshwa wa Zantel 4G,” alisema Muga.   Aliongeza kuwa Zantel inaendelea kuboresha mtandao ili kwenda na kasi ya ulimwengu kidigitali, ikiwamo kufanya uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano ikiwamo minara mipya ya simu hasa kwenye maeneo ya vijijini ili kuwafikia watu wengi zaidi.   “Nia yetu ni kuendelea kuboresha mtandao wetu ili mawasiliano yapatikane Zanzibar yote kwa kasi ya 4G na kumuwezesha mtumiaji kupata mawasiliano bora na ya haraka,” alisema Muga na kuongeza:   “Ni wazi kuwa kupitia simu ya mkononi tu unaweza kufanya mambo mengi sana kwa haraka na urahisi zaidi. Mfano, kukata tiketi za safari mbalimbali kama boti, kununua na kuuza bidhaa mbali popote ulimwenguni kwa muda mfupi,kupata elimu, kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki.”   “Kwanza kabisa, kupitia intaneti ya 4G mteja wetu anapata spidi ya kasi ambayo inamuwezesha kufanya shughuli zake mtandaoni haraka na kwa urahisi zaidi. Hii inamfanya mtumiaji kupata taarifa kwa haraka zaidi tofauti na yule anayetumia 3G,” alisema.   Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Zantel Kanda ya Pemba, Said Masoud Ali, alisema mpango ni kuhakikisha kila mtu anafikiwa na mtandao wa 4G ikiwamo kuwawezesha watu kupata simu za bei nafuu.   “Tumeleta simu ambazo zina uwezo wa 4G na tunaziuza kwa bei nafuu ambapo tunatoa punguzo hadi asilimia 5 pamoja n GB 2 bure… hii inasaidia kila mtu kupata mtandao wetu wa 4G,” alisema Ali.

Chanzo: ippmedia.com