Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya vifaranga Milioni 21 vya samaki vimezalishwa TZ

6661bc3f5d9f03c31caab8275d5c39fa Zaidi ya vifaranga Milioni 21 vya samaki vimezalishwa TZ

Wed, 3 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Serikali imesema  katika mwaka 2020  jumla ya vifaranga 21,676,187 vya samaki vimezalishwa kutoka katika vituo vya serikali na vya  binafsi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema vituo binafsi vimezalisha samaki 17,529,347 na vituo vya Serikali vimezalisha samaki  4,146,840 ikilinganishwa na vifaranga 17,301,076 vilivyozalishwa mwaka 2019 sawa na ongezeko la asilimia 25.3.

Ndaki amesema lengo la serikali ni kuzalisha vifaranga milioni 30 mwaka huu ambapo Vituo na Taasisi za Serikali vitazalisha vifaranga milioni nane  na sekta binafsi kuzalisha vifaranga milioni 22.

FISI 22 WAUAWA, WAMEUA WATU WATANO, MAMA AMWAGA MACHOZI “LIFISI LIMEKULA MTOTO WANGU”

Chanzo: millardayo.com