Menu ›
Biashara
Thu, 30 Jun 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Taasisi ya China Cassava Association imepanga kuanza kununua Tani 60,000 za muhogo mkavu kutoka Tanzania kila mwezi kuanzia mwakani 2023, Taasisi hiyo imeeleza utayari wake kushirikiana na sekta binafsi nchini Tanzania kuongeza uzalishaji wa muhogo (commercial farming).
Makubaliano hayo ya ununuzi wa muhogo mkavu yamefanyika katika Mkutano wa Balozi wa Tanzania nchini China? Mbelwa Kairuki na Mwenyekiti wa China Cassava Assocation, Dai Wei.
Taasisi hiyo imeeleza itakapoanza kununua muhogo itakuwa ikituma Meli zake kubeba bidhaa hiyo kupitia bandari ya DSM na Mtwara
Chanzo: www.tanzaniaweb.live