Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya tani 12,000 za ufuta kuuzwa Songwe

Ufuta Pc Data Zaidi ya tani 12,000 za ufuta kuuzwa Songwe

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Songwe Solomon Itunda amesema changamoto zilizojitokeza mwaka Jana kwenye uuzaji wa ufuta kupitia stakabadhi ghalani wameshaanza kuzitatua ikiwemo suala ya uchache wa maghala,vifungashio na kuimarisha zoezi la uuzaji wa ufuta ili faida iweze kuwa zaidi ya msimu uliopita huku matarajio yakiwa ni kuuza zaidi ya bilioni hamsini (Bil.50) kulingana na uzalishaji wa ufuta kuwa mkubwa.

katika kikao kilichifanyika hivi mbalimbali kilichohusisha wadau wa sekta ya ufuta Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songwe Abraham Sambila alianisha matarajio ya msimu huu ikiwa ni kupata tani zaidi ya elfu kumi na mbili(12000) ikiwa ni zaidi ya tani wa msimu uliopita.

Wilaya ya Songwe inatarajia kuwa na mnada wa kwanza wa uuzaji wa zao la ufuta kupitia stakabadhi ghalani Mei 5 mnada ambao unasubiliwa kwa shauku na wakulima wa ufuta katika Wilaya hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live