Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya 95% ya mafuta ya kula hupitia Mbweni

 Mafuta Ya Kula Hupitia Mbweni Zaidi ya 95% ya mafuta ya kula hupitia Mbweni

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameelekeza Mamlaka ya Bandari kufanya Maboresho ya Miundombinu ya Bandari ndogo ya Mbweni Baada ya Rais Samia kurasimisha rasmi Bandari hiyo.

Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara kwenye Bandari hiyo ambapo amewataka TPA Na TARURA kuandaa michoro, gharama Za barabara Na miundombinu ya bandari hiyo ili biashara zifanyike pasipo usumbufu.

Aidha Makalla amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kurasimisha Bandari hiyo Baada ya muda mrefu kutumika Kama Bandari bubu na kusababisha Serikali kukosa Mapato.

Hata hivyo  Makalla amesema Asilimia 95 ya Mafuta ya kula yanapita Katika bandari hiyo hivyo ni lazima maboresho yafanyike ambapo ametoa wiki moja kwa Mamlaka ya Bandari kuweka kibao Cha kuonyesha Bandari hiyo.

Katika ziara hiyo RC Makalla amepokea changamoto mbalimbali kutoka kwa Wafanyabiashara wanaotumia Bandari hiyo na kuahidi kuzipatia ufumbuzi wa haraka. Pamoja na hayo  Makalla ametoa wito kwa Wafanyabiashara wanaotumia Bandari hiyo kutokumuangusha Rais Samia kwa kuhakikisha wanalipa mapato na kufuata sheria, kanuni na taratibu.

Ikumbukwe kuwa Bandari ndogo ya Mbweni imerasimishwa rasmi tarehe 06/ 05/2022 na Rais Samia Suluhu Hassan na Sasa inatoa huduma Kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live