Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ZRA yatangaza kodi mpya za majengo

Tozo Ghorofa Zanzibar (600 X 342) ZRA yatangaza kodi mpya za majengo

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), Yusuph Juma Mwenda amesema kodi mpya za majengo zitakazoanza kutumika Zanzibar kuanzia November 30,2023, kwa upande wa nyumba za makazi zitatozwa kwa wenye ghorofa pekee na watatozwa Elfu 10 kwa mwaka lakini nyumba zisizo za ghorofa hazitolipiwa kodi.

Mwenda amesema hayo alipokutana na Wenyeviti wa Mitaa wa Magharibi A, Magharibi B na Wilaya ya Mjini ambapo amesema kodi hizo mpya zitaanza kulipwa November 30,2023, kauli ya Mwenda inakuja baada ya kuibuka kwa uvumi uliozua taharuki Zanzibar kwamba nyumba zote zitaanza kutozwa kodi.

“Wengine wanawatia Watu hofu kuwa nyumba zote zitalipiwa kodi sio kweli, wanaolipa ni wenye ghorofa pekee Tsh. elfu 10 na italipwa mara moja kwa mwaka, ikitokea Mtu hana uwezo wa kulipa ataandika barua na kuonesha sababu ikithibitika tutamuongezea alipe kidogokidogo na watalipa kwa control number kupitia mtandao”

Hii ni mara ya kwanza kwa Zanzibar kuanza utaratibu wa kutoza kodi kwa nyumba za makazi, kabla ya hapo ni Hotel na majengo mengine ya biashara pekee ndio yalikuwa yanatozwa kodi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live