Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ZBS: Bidhaa zenye ubora kutambulika kimataifa

ZBS VIWANGO ZBS: Bidhaa zenye ubora kutambulika kimataifa

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeelezwa kuwa kutolewa kwa kibali cha huduma za ithibati ya viwango kutoka Jumuiya ya maendeleo ya Afrika Kusini SADCAS kwa taasisi ya Viwango Zanzibar kuitafungua fursa mbalimbali za kutambulika kwa bidhaa zenye alama ya ubora kutoak ZBS katika soko la Kimataifa

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Yussuf Majid Nassor wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisi kwake Marhubi, baada ya kupokea cheti cha ithibati ya ubora kutoka SADCAS jambo ambalo litafungua fursa mbalimbali za masoko kwa wadhalishaji na wajasiriamali ambao watakidhi viwango na kupatia alama ya ubora kutoka ZBS

Amesema hatua hiyo kubwa ya kutambulika kimatiafa inatokana na juhudi za makusudi za serikali ya awamu ya nane chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika kuhakikisha inawekeza katika kujenga maabara kubwa za kisasa na kuajiri wataalamu waliokidhi viwango

Chanzo: www.tanzaniaweb.live