Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ZBR kutumia risiti za kielektroniki

6250ec577864fd6cfb07dcf816d80465.png ZBR kutumia risiti za kielektroniki

Wed, 29 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

BODI ya Mapato Zanzibar (ZRB) inakusudia kuanza kutumia mashine za kutoa risiti kwa njia ya kielektroniki (EFD) kudhibiti upotevu wa mapato pale wananchi wanapofanya manunuzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa ZRB, Joseph Abdalla Meza alisema maandalizi ya kuanza mfumo wa utoaji wa risiti kielektroniki yamekamilika kwa watendaji na maofisa wa bodi kupewa mafunzo.

Alisema mfumo wa utoaji risiti kielektroniki unatarajiwa kuanza kufanya kazi Septemba.

“Nawajulisha wananchi na wafanyabiashara ZRB inatarajiwa kuanza kutumia mfumo wa utoaji wa risiti kwa njia ya kielektroniki kwa wafanyabiashara kuanzia mwezi Septemba ili kudhibiti upotevu wa fedha za serikali,” alisema.

Ofisa Uhusiano wa ZRB, Shaaban Yahya alisema kwa kuanzia risiti za kielektroniki zitatolewa kwa wafanyabiashara wakubwa, biashara za jumla na vituo vya mafuta.

Alisema kutokana na matumizi ya risiti za kielektroniki bodi hiyo inakusudia kupata Sh bilioni 50 kwa mwaka zilizokuwa zikipotea kutokana na kufanya manunuzi bila kudai risiti.

Baadhi ya wafanyabiashara wameukaribisha mashine za kielektroniki wakiamini kiasi kikubwa utaondoa malalamiko na usumbufu uliokuwa ukifanywa na watendaji wa taasisi hiyo.

“Mimi nimefurahishwa na ujio wa mashine za kielektroniki ambazo zitatusaidia kuondoa malalamiko yaliyokuwa yakitupata mara kwa mara kutoka kwa watendaji wa bodi ya mapato,” alisema mfanyabiashara, Issa Haji.

Chanzo: habarileo.co.tz