Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yapata shavu la kukitangaza kinywaji cha GSM

Gsm Yanga Kinywaji Yanga yapata shavu la kukitangaza kinywaji cha GSM

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jana Julai 30, 2024 ambapo GSM Group of Companies leo wanayofuraha ya kupanua wigo wa mahusiano na Klabu ya Yanga ambapo wametangaza rasmi kampuni yao mpya ya vinywaji ya GSM kuingia mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo.

“Kwa niaba ya GSM Group tunayo furaha ya kutangaza rasmi kuwa tumepanua wigo wa mahusiano yetu na klabu ya Yanga SC, tunatangaza rasmi kuwa kampuni mpya ya vinywaji ya GSM imeingia mkataba wa miaka mitano na klabu ya Yanga SC, na mkataba huu una thamani ya Tsh bilion 1,” amesema Benson Mahenya CEO wa GSM Group.

“Tunashukuru sana Uongozi wa GSM Group kwa kutambua umuhimu wa kuongeza nguvu ya udhamini kwa klabu yetu, Kampuni hii ya vinywaji visivyo na kileo kama juisi, soda na maji itakuwa sehemu ya wadhamini wetu kwa kipindi hicho cha miaka mitano.

“Leo tumekuja hapa kuwatangazia wadhamini wetu kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi, mdhamini mkuu wa wiki ya mwananchi ni benki ya CRDB, hata hivyo tumeongeza washirika wengine ni Benki ya Equity pamoja na GSM Beverage,” Simon Patrick Mkurugenzi wa Sheria Klabu ya Yanga SC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live