Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yajue maeneo yenye uwekezaji mkubwa nchini

Uwekezajiiiii Sera Yajue maeneo yenye uwekezaji mkubwa nchini

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: mwanachidigital

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema uwe-kezaji katika kila sekta unalipa isipokuwa yapo mae-neo ya kipaumbele ambayo nchi inatamani uwe-kezaji zaidi, hivyo kuyawekea motisha.

Kwa mujibu wa TIC mwekezaji atakayejitokeza atanufaika na motisha zaidi katika maeneo ya sekta za kipaumbele kama vile viwanda vya kuzalisha su-kari, mbolea, mafuta ya kula, ngano na mbegu.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri amesema pamoja na Sheria ya Uwekezaji Tanzania mwaka 2022 kuweka viwango sawa kwa uwekezaji mkubwa, bado kuna fursa ya mwekezaji wa maeneo hayo kuomba motisha kwa maeneo gani anayoona inafaa ili kurahisisha uwekezaji wake.

Katika mahojiano maalumu ofisini kwake, Teri alisema Tanzania inatoa kipaum-bele kwa uzalishaji wa bidhaa ambazo inatumia kiasi kikubwa cha fedha kuziagiza nje na TIC ina ardhi kwa ajili ya kuwezesha wanaotaka kuwekeza katika uzalishaji wa bidhaa hizo hususani za kilimo.

Chanzo: mwanachidigital