Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wwafanyabiashara wa mahindi wazidi kuneemeka

Mahindiy Bei ya Mahindi inaendelea kupanda katika soko la ndani

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Neema yaendelea kuwashukia wakulima na wafanyabiashara wa mahindi, baada ya bei ya zao hilo kuendelea kupanda katika kipindi cha mwaka mmoja unaoishia Januari 2022.

Kwa mujibu wa ripoti ya mapitio ya uchumi kwa mwezi Februari 2022 (Monthly economic review) iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), bei ya jumla ya zao hilo (gunia la kilo 100) imeongezeka hadi kufikia Sh65,864 katika mwaka unaoishia Januari 2022 kutoka Sh56,866 iliyotumika kipindi kama hicho mwaka jana.

Hilo ni sawa na ongezeko la asilimia 13.7 au sawa na kusema wakulima wataweka kibindoni Sh8,997 kwa kila gunia la kilo 100 ambayo mwaka jana wasingeipata.

Hata hivyo, wanunuzi wa zao hilo watalazimika kutoboa zaidi mifuko yao na hivyo wanaweza kupata maumivu.

Mahindi ni miongoni mwa mazao makuu ya chakula yanayojumuisha mchele, maharage, viazi mviringo, mahindi, mtama, uwele na ulezi.

BoT katika ripoti hiyo imeeleza kuwa tangu Septemba 2021 bei ya mahindi imekuwa ikipanda kwa miezi minne mfululizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live