Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara yauza madini ya Tsh.Trilioni 8.3

Madini Ofii Geita Wizara yauza madini ya Tsh.Trilioni 8.3

Thu, 10 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini nchini Tanzania Dotto Biteko ameyazungumzia mafanikio mbalimbali kwenye Wizara hiyo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja toka Rais Samia akalie kiti cha Urais wa Tanzania ambapo sehemu ya mafanikio hayo ni kuweka historia ya kufikisha mauzo ya Trilioni 8.3.

"Katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya awamu ya sita sekta ya Madini imeweka historia kwa kushuhudia mauzo ya moja kwa moja yenye thamani ya shilingi Trilioni 8.3 kutokana na mauzo ya madini ya aina mbalimbali, mauzo hayo yanatokana na madini ya dhahabu, madini ya fedha, madini ya shaba, makaa ya mawe, madini ya kinywe, madini ya vito na madini ya ujenzi wa viwandani"

"Kutokana na biashara ya madini hayo, Wizara imekusanya shilingi Bilioni 597.53 kama maduhuli ya Serikali yaliyokusanywa kupitia Wizara" ——— Dotto Biteko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live