Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara yatoa tahadhari uwepo samaki wenye sumu

Samaki Bunju Sumu Wizara yatoa tahadhari uwepo samaki wenye sumu

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WIZARA ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, imesema samaki aina ya bunju ni hatari kutokana na kuwa na sumu hivyo imewataka wavuvi kuchukua tahadhari ya hali ya juu wakati wanapomvua na kumtengeneza kwa ajili ya matumizi ya kitoweo.

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Shamata Shaame Khamis alisema hayo jana wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Kojani, Hassan Hamad Omar (ACT-Wazalendo).

Mwakilishi huyo alitaka kufahamu elimu inayotolewa kuhusu samaki aina ya bunju ambaye amekuwa tishio.

Khamis alisema samaki huyo ni maarufu katika mwambao wa Afrika Mashariki na amekuwa akitumiwa kama kitoweo kwa wananchi wengi.

Hata hivyo, alisema samaki huyo anapovuliwa, hulazimika kuchunwa na kuondoa gamba lake huku tahadhari zikichukuliwa kuhakikisha sehemu yenye sumu kali haitumbuki.

Alisema Wizara ya Kilimo pamoja na Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu haina nia ya kupiga marufuku uvuvi wa samaki huyo

“Wavuvi wenyewe wanatakiwa kuchukua tahadhari wakati wanapovua samaki huyo kabla ya kula,'' alisema.

Kwa nyakati tofauti kwa upande wa Zanzibar samaki aina ya bunju amesababisha vifo kwa wananchi baada ya wavuvi kushindwa kumtengeneza vizuri kwa ajili ya kula na kusababisha kutumbuka kwa 'shiri' lake na kuzalisha sumu. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live