Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara yataka kuwepo kwa 'Cold Room' kunusuru kuoza kwa mazao

Kilimo Cha Parachichi Scaled Wizara yataka kuwepo kwa 'Cold Room' kunusuru kuoza kwa mazao

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, ameuagiza Uongozi wa Songwe Airport kujenga chumba maalum kwa ajili ya kuhifadhia mazao na vitu vingine vinavyoharibika kutokana na joto (Cold room) katika uwanja huo ili kuwanufaisha Wasafirishaji bidhaa mbalimbali hususani mazao kwenda Mikoani na Nchi mbalimbali za nje.

"Mfano maparachichi yakitoka shambani kule Njombe au Tukuyu yaje yafike Songwe Airport ni siku ngapi kwamba yakafike yanakoenda si yatakuwa yameharibika?, nimemuuliza Meneja cold room iko wapi hakuwa na majibu, mnataka parachichi ziozee Airport?, nimeagiza mchakato wa kujenga cold room uanze mara moja”.

Kihenzile amesema hayo wakati akitoa ripoti ya majumuisho ya ziara yake ambayo ameifanya Mkoani Mbeya, ambapo amesema baada ya kutembelea uwanja huo wa ndege wa Songwe licha ya kukosa cold room lakini amepongeza juhudi zinazofanyika katika kujenga uwanja huo kwa ubora kama inavyotakiwa.

Kihenzile amesema Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imeridhishwa na mwenendo wa ujenzi na maboresho yanayoendelea kufanyika katika uwanja huo wa Ndege wenye hadhi ya Kimataifa wa Songwe Mkoani Mbeya ikiwemo jengo kubwa na la kisasa kwa ajili ya abiria ambalo limekamilika kwa 98%.

Uwanja huo unahudumia Mikoa saba kuanzia Katavi, Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Ruvuma na Iringa ambapo Kihenzile ameitaka pia Mamlaka ya viwanja vya ndege kuja na mkakati wa kuhakikisha wanaongeza idadi ya abiria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live