Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara yaipa ASA mitambo ya kilimo

Asaspiic Data Wizara yaipa ASA mitambo ya kilimo

Fri, 13 May 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Wizara ya Kilimo imeipatia Wakala wa Mbegu za Kilimo Tanzania (ASA) mitambo ya kisasa ya kulima, kupulizia dawa wadudu na kupanda ikiwa na thamani ya zaidi ya Sh400 milioni kwa ajili ya kuongeza tija katika uzalishaji wa mbegu za mazao ya kimkakati nchini.

Akizungumza katika mafunzo kwa maafisa kilim0, mafundi mitambo na madereva wa mitambo kutoka ASA Mei 12, Mkurugenzi wa uzalishaji wakala hiyo, Justine Ringo amesema wametoa mafunzo kwa ajili ya kujua namna ya kutumia mitambo hiyo kwa ufanisi.

“Mitambo tuliopokea inaenda kuongeza ufanisi wa uzlishaji mbegu za mazao ya kimkakati kwa mbegu za alizeti, ngano katika shamba la mbegu bora za kilimo la Ngaramtoni Arusha na shamba ya Msimba Kilosa litakalokuwa na uzalishaji wa mbegu bora kwa mazao ya kimkakati alizeti na mengine,” alisema Ringo.

Ringo amesema mazao mengine ya kimkakati ni pamoja na mahindi, soya ambapo mpango wa wakala huyo inatarajia kulima hekta 1,500 hadi hekta 2,000 za mbegu bora za alizeti katika shamba la Msimba wakati Arusha kulimwa mbegu bora za kilimo kwa mazao ya alizeti na ngano hekta 450 hadi hekta 600.

Mmoja wa maofisa kilimo shamba la wakala wa mbegu la Mwele Tanga, Rehema Anthony amesema kupatiwa mafunzo kwa makundi hayo yatasaidia kila mmoja wake kuwajibika ipaswavyo bila ya kuwa na changamoto kutokana na mitambo hiyo kuwa ya kisasa zaidi tofauti na ile ya awali.

“Kila mmoja atawajibika kiufasaha kutumia hii mitambo kwa kusimamia shughuli za upandaji, uwekaji dawa shambani na kulima kwani wakati madereva wa kuendesha mitambo wao kama maafisa kilimo watahitaji kutoa maelekezo ya kitalaamu katika kuweka dawa na kupanda,” amesema Rehema.

Fundi mitambo msaidizi shamba la mbegu Msimba Kilosa, Bakari Kissingi amesema mafunzo hayo yamewapa uelewa wa kufunga na kufungua vipuri, kutengeneza na kubadilisha vifaa.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz