Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara yabaini sababu kuadimika kwa soda nchini

Soda Wizara yabaini sababu kuadimika kwa soda nchini

Mon, 24 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dk. Ashatu Kijaji, amefanya ziara mkoani Shinyanga na kutembele viwanda vya mkoani hapo kwa ajili ya kutazama utendaji kazi na kusema kuwa sababu ya kuadimika kwa vinywaji baridi ni kutokana na kuadimika kwa sukari ya viwandani.

Alisema mwaka jana kuanzia Oktoba hadi Januari mwaka huu, kulitokea tatizo la baadhi ya vinywaji baridi kupanda bei ghafla, ndipo serikali kupitia tume ya ushindani, ikabidi ifanye uchunguzi ili kubaini tatizo liko wapi, na kupata majibu ya kasi ya uzalishaji vinywaji hivyo ilivyopungua, kutokana na kuadimika kwa Sukari ya viwandani.

Alisema uchunguzi huo ulibaini kuwa licha ya kuadimika kwa Sukari hiyo ya viwandani, lakini wazalishaji wa vinywaji baridi hawakupandisha bei, isipokuwa mawakala wa usambazaji na wafanyabiashara ndiyo waliopandisha bei, na kuonya tabia hiyo isijirudie tena na watakaobainika watachukuliwa hatua.

“Baada ya kupanda bei ghafla ya vinywaji baridi, serikali kupitia tume ya ushindani ilibidi tufanye uchunguzi na kubaini vinywaji baridi vimeadimika sababu ya kupungua kasi ya uzalishaji kutokana na kutopatikana kwa Sukari ya viwandani au sababu ya ukosefu wa Makasha ya kusafirishia Sukari hiyo kuja hapa nchini,”alisema Kijaji.

“Tume ya ushindani ilibaini pia tatizo la kupanda kwa bei ya vinywaji baridi halitokei kwa wazalishaji, bali ni Mawakala wa usambazaji na wafanyabiashara ndiyo waliopandisha bei ya vinywaji baridi mara baada ya kuona bidhaa hiyo imeanza kuadimika sokoni,”aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live