Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya madini kuja miradi mikubwa ya kimkakati

MAVUNDEEEEEE Wizara ya madini kuja miradi mikubwa ya kimkakati

Wed, 14 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WIZARA ya Madini kwa kushirikiana na kampuni mbalimbali za uchimbaji na uchakataji madini inatarajia kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati itakayohusisha mnyororo mzima katika sekta ya madini.

Kaimu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Ramadhan Lwamo amebainisha hayo wakati akiwasilisha taarifa kuhusu hali ya ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaopaswa kutoa maeneo yao ili kuruhusu uendelezaji wa leseni za uchimbaji wa madini nchini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Mhandisi Lwamo amesema Tume ya Madini ilitoa leseni za uchimbaji wa madini wa kati na mkubwa katika maeneo mbalimbali nchini ambayo yamekuwa yakihitaji taratibu za kuhamisha wananchi ili kupisha utekelezaji wa miradi husika.

Ametaja miradi hiyo kuwa ni wa uchimbaji madini ya nikeli wa Kabanga, mradi wa uchimbaji mkubwa wa SMCL mkoani Mwanza, mradi wa uchimbaji madini ya kinywe wa Faru Graphite mkoani Morogoro, mradi wa uchimbaji madini ya mchanga mzito wa Baharini (Heavy mineral sands).

Mingine ni mradi wa uchimbaji madini ya kinywe wa Bunyu, Nachu na Chilalo mkoani Lindi na Epanko mkoani Morogoro.

Kwa upande wake Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema wizara yake inaahidi kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha kampuni zinakamilisha taratibu za ulipaji wa fidia kwa wananchi pamoja na kuendeleza miradi husika na kusimamia utekelezaji wake.

Waziri Mavunde ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa ushauri wake makini ambao imekuwa ikiutoa katika nyakati tofauti na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo na ushauri wote wa kamati hiyo katika kuhakikisha sekta ya madini inaendelea kukua kwa kasi na hatimaye kuchangia ipasavyo katika ukuaji wa uchumi wa Taita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live