Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya kilimo kuwezesha upatikanaji masoko kidijitali

Handeni Mazao.png Wizara ya kilimo kuwezesha upatikanaji masoko kidijitali

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Kilimo imesema inajipanga kutoa mafunzo ya upatikanaji wa masoko kidijitali kwa wataalamu wa kilimo katika ngazi zote ili kuimarisha uhakika wa chakula nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana Jumapili Aprili 28, 2024 na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akizungumzia namna ya kuwanufaisha wakulima kupitia sekta hiyo.

"Wizara ya Kilimo imekuwa na mkakati wa kutoa mafunzo kuhusu Mfumo wa Crop Stocks Dynamics System (CSDS) kwa watalaamu wa kilimo katika ngazi ya halmashauri na sekretarieti za mikoa ili kuimarisha usalama wa chakula na upatikanaji wa masoko nchini.

"Huu ni mfumo wa kidigitali wa kusajili ghala, masoko, vituo vya ukaguzi wa mazao na wafanyabiashara ili kufuatilia uhifadhi wa mazao ya kilimo kwenye ghala na usafirishaji wa mazao ya kilimo, kisha ufuatiliaji wa mazao yanayoingia kwenye masoko ya walaji.

“mfumo huu una sehemu tatu ambazo ni usimamizi wa mazao ya kilimo kwenye ghala, usimamizi wa mazao ya kilimo yanayoingia sokoni na ufuatiliaji wa mazao ya kilimo yanayosafirishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine," amesema Bashe.

Bashe amesema mfumo huo unasaidia kutoa taarifa za usajili wa masoko, ghala na vituo vya ukaguzi wa mazao ya kilimo unaowezesha kufahamu takwimu sahihi za kiasi cha mazao yanayoingia na kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live